Habari

Kimbunga Eloise chapiga Msumbiji na kuleta mafuriko

Baadhi ya maeneo ya kati ya taifa la Msumbiji yamekumbwa na mafuriko baada ya kimbunga Eloise kupiga eneo lililo karibu na mji wa Beira na upepo wenye kasi ya kilomita 160 kwa saa.

Limpopo vigilant as cyclone Eloise lashes Mozambique - SABC News - Breaking  news, special reports, world, business, sport coverage of all South African  current events. Africa's news leader.

Beira ilipokea milimita 250 za mvua katika kipindi cha saa 24 , kulingana na Taasisi ya kitaifa ya hali ya hewa nchuni humo INAM.

Baadhi ya maafisa na mashirika ya misaada yanachunguza kiwango cha uharibifu huo ili kuweza kuwasaidia walioathirika, na kujaribu kurudisha umeme na mawasiliano ambayo yalikatwa katika baadhi ya maeneo. Watu wameuawa kulingana na maafisa.Rain falling

Kimbunga hicho hatahivyo kimeshushwa hadhi na kutajwa kuwa dhoruba ya kitropiki na kilitabiriwa kuelekea Zimbabwe na kaskazini mwa Afrika Kusini mataifa ambayo tayari yamekumbwa na mvua kubwa.

Chris Neeson , ambaye anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa katika mji wa Beira alisema: Ilikuwa vigumu kulala kutokana na kelele na hofu. Nilisikia upepo mwingi na mvua ikinyesha mapema alfajiri.

A man using a bucket to clear water from his house

”Maji yaliingia katika nyumba yangu , pamoja na mawe, na majani ambayo yalikuwa yametoka katika nyumba za majirani wangu. Umeme umekatika tangu usiku uliopita na tumeshindwa kupiga simu”.

”Nilipotoka nje , maji yalikuwa yametapakaa kila mahali hadi katika magoti yangu, huku miti, nyaya za umeme, paa na ua zikiharibiwa na kusafirishwa katika barabara. Nashukuru Mungu mvua imepusa .Sikudhania nitaogopa maji lakini hii ilikuwa inatisha”, alisema.

Wakaazi wa Beira, mji wa pili kwa ukubwa nchini Msumbiji ukiwa na idadi ya watu wapatao 500,000, wanajaribu kuusafisha.familia ikiwa imesimama nje ya nyumba yao iliokumba na mafuriko

Zaidi ya nyumba 1,000 zimeangamizwa na nyengine 3,000 zikiharibiwa vibaya kulingana na Antonio Beleza, kutoka Taasisi ya usimamizi wa majanga .

Kochi likiwa ndani ya chumba kilichokumbwa na mafuriko

Alisema kwamba zaidi ya watu 160,000 waliathiriwa moja kwa moja. Baadhi yao wanajaribu kuokoa chochote kutoka katika nyumba zao zilizokumbwa na mafuriko.Watoto wanatembea katika barabara yenye mafuriko huku nguo za kulalia zikianikwa ili kukauka

Miti , na nyaya za umeme pamoja na mabango ya matangazo yalisombwa na nguvu za upepe huo.Bango la matangazo lililoanguka barabarani

Baadhi ya mito katika eneo hilo pia imevunja kingo zake.Mtu amesimama katika daraja ambalo mto wake umevunja kingo zake

Maeneo mengi ya Msumbiji ya kati yapo chini ya maji . Mengi kati ya maeneo hayo ni yale ya mashambani ambapo kuna hofu kwamba watu wengi watapoteza mazao yao .Picha ya juu ya eneo lililokumbwa na mafuriko

Viwango vya maji vilikuwa vya juu kabla ya kimbunga hicho kupiga siku ya Jumamosi.

Eneo hilo linaendelea kujiponya kutokana na vimbunga viwili kile cha Idai na Kenneth ambavyo vilikumba taifa hilo mwaka 2019 , na kuwaua mamia huku maelfu wakiwachwa bila makao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents