Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari
Kinachoendelea Oysterbay Polisi alipo Kizz Daniel, bado yupo ndani
Team ya Bongofive bado ipo hapa kituo cha Polisi cha Oysterbay kujua kinachoendelea baada ya kukamatwa staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Kizz Daniel alasiri ya leo.
Kizz Daniel amekamatwa na waandaaji wa show yake ambayo ilitakiwa kufanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Next Door Arena Masaki Jijini Dar Es Salaam na bado haijawekwa wazi hasa tatizo lilikuwa nini msanii huyo kutotokea jukwaani.
Waandaaji wa Show hiyo Str8upvibe walishaomba msamaha lakini mengi yameongelea kuwa msanii huyo alisahau nguo ingawa uongozi bado hujathibitisha.
Bado yupo ndani kituo cha Polisi na haijajulikana kipi kinaendelea na je atatoka leo au atalala polisi.