Habari

King Majuto awapa ‘tuition’ ya uchekeshaji John Walker na Ras Lion

Mchekeshaji mkongwe nchini King Majuto ameamua kuwasaidia wasanii wa Bongoflava ambao wamepotea kwenye ramani ya muziki huo na kuwafundisha fani ya uchekeshaji ili kuongeza wasanii wa fani hiyo.

SAM_1362

King Majuto amesema ni kipindi kirefu amekuwa akiona vipaji vya wasanii kadhaa ambao licha ya kupotea kwa muda katika gemu ya muziki wanahitaji msaada. Kwa kuanza Mzee huyo ameamua kuwachukua John Walker na Ras Lion waliowahi kutamba nchini kwa uwezo wao wa kuimba nyimbo kwa lafudhi za Kijaluo, kisukuma na kama mtu aliyelewa.

Majuto alisema lengo lake ni kuona anawaandaa wasanii wengi zaidi kwenye fani ya uchekeshaji ili aweze kujivunia atakapostaafu kuchekesha. Pamoja na John Walker na Ras Lion , Majuto ana mpango wa kuongeza wasanii wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents