Burudani

Koba amshutumu Afande Sele kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ‘Watu Pori’ Afande amshauri afanye yake kama Ditto

Mfalme wa Rhymes, Afande Sele, ameshtumiwa kuwa ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi la Watu Pori licha ya kutafutwa mara kwa mara na wasanii wenzake akiwemo, MC Koba kwa nia ya kulirudisha tena kundi hilo kwenye game.

DSC00272

Akiongea na ‘Chumba cha Sindano’, kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio, Bomba FM Mbeya, MC Koba amesema anaumia kuona kundi hilo limevunjika.

“Kiukweli hakuna mtu anayependa mvunjiko. Mimi kama mimi binafsi roho inaniuma sana kwa sababu nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kupigania uwepo wa kundi la Watu Pori, lakini kushindikana kwake au ugumu wake unaletwa na brother tunayempa nafasi. Niseme nini, tunampa dhamana ya kutuongoza kwa sababu Koba hawezi kuwa kiongozi, Ditto hawezi kuwa kiongozi,”alisema Koba.

MC Koba anadai kuwa Afande Sele ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo.

“Afande alikuwa anatutupia sisi mzigo unajua, vijana ndio hawataki, vijana ndio hawataki, sasa mimi nikasema kwamba any way kwa sababu nimesikia rumors za namna hiyo kutoka kwa watu wengi, hata mimi watu walikuwa wananipigia simu kwanini mnafanya hivyo, ‘muziki unashuka, Watu Pori wameshuka’ na vitu kama hivyo unajua. Kwa hiyo mimi nikaona kwa sababu napenda umoja wetu ngoja basi tufanye track.”

Hata hivyo, Ditto alikuwa na mtazamo tofauti na Koba.

“Sidhani. Unajua Watu Pori, watabaki, Watu Pori ni mtu yeyote ambaye yupo katika zile himaya, haya mambo mengine yanayoendelea ni katika kujijenga tu sisi wenyewe umeshanifahamu. Lazima Ditto awe Ditto mwisho wa siku na Afande kama Afande mwisho wa siku. Mimi sidhani kama kuna tofauti namna tunavyoishi kila siku binafsi mimi, hatufanyi vitu kwa sababu ya urafiki au labda ya udugu au sijui ya nini,” alisema Ditto.

“Siku hizi ni biashara, soko likihitaji yaani mimi binafsi nikiona soko linahitaji Watu Pori kufanya biashara, biashara imekubali nini kitakachonirudisha nyuma, au Koba nini kitakachomrudisha nyuma au Afande nini kitakacho mrudisha nyuma. Soko la sasa linahitaji Afande Sele atoe nyimbo zake, Koba atoe nyimbo zake basi ndo hicho ndo kikubwa kwa hiyo mimi sidhani kama ikitokea biashara kwamba biashara inalazimisha ufanye kitu fulani kisifanyike hakuna hicho. Hatufanyi muziki kwa ajili ya udugu, udugu unakuwepo lakini hauingiliani na masuala yetu ya kibiashara.”

Alipoulizwa kuhusiana na kauli ya Koba, Afande alisema:

“Kundi sio msingi, kwanza sina hata stori kwani lazima kuwa na kundi mimi sina kundi, Koba nilimchukua kama mtoto yatima, Dito kama mtoto yatima nimewalea nyumbani kwangu basi. Kwa hiyo mimi nilikuwa kama bridge kwa sababu kimoyoni Koba hakuwepo alikuwa kama wale watoto wa mitaani ambao wana matatizo na mimi kawaida yangu ni kuwasaidia vijana. Kwa hiyo nikawachukua kipindi kile nikawatengenezea kundi la Gheto Boys likasambaratika, nikatengeneza Watu Pori likaja kusambaratika sasa hivi kila mtu ana maisha yake sio muda wa kutengeneza makundi, makundi kwa kulipwa hela gani bwana
Kwanza toka zamani nilikuwa sina kundi isipokuwa nilikuwa naishi nao pamoja isipokuwa niliwatafutia kitu cha kuwauza ila wao walishindwa kutulia na kuelewa.”

Afande Sele anadai alitumia gharama nyingi kuwatengeneza Ditto na Koba lakini walikuja kumkimbia. “Baadae wamejiona wamejua wamekimbia wenyewe hakuna aliyewafukuza.”

Rapper huyo mkongwe anamsihi Koba kuwa, naye atazame maisha mapya.

“Sasa inatakiwa naye apiganie maisha kama mwenzake Ditto anafanya maisha magumu japo sisikii anafanya muziki wowote wala sijui muziki anaofanya, lakini namwona anaishi yuko mjini anakaa vizuri anatembelea gari japo sijui naye anafanya nini. Koba anapaswa afikirie afanye nini katika maisha yake afanye shughuli zake au muziki au kitu kingine ili mimi Afande Sele nibaki kama Afande Sele sitaki kundi na sina kundi. Kwa hiyo hata Koba alivyorudi nilivyomshirikisha kwenye wimbo Amani na Upendo ule ni wimbo wangu. Lakini sio kwamba tunarudisha kundi cha msingi uwaelimishe madogo kuwa makundi ni kudhihirisha woga.

By: Greyson Chris Bee (Bomba FM, Mbeya)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents