Habari

Korea Kaskazini yafanya jaribio jingine la kombora tofauti na kawaida, safari hii halijatoka ardhini

Korea Kaskazini imethibitisha kufanya jaribio la kurusha aina mpya ya kombora, baada ya kufanikiwa kurusha makombora ya masafa mafupi tangu mwezi Mei.

What appears to be a submarine-launched ballistic missile (SLBM) flies in an undisclosed location in this undated picture released by North Korea's official news agency

Jaribio hili nchini humo ni la kumi na moja kwa mwaka huu ambapo makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia yanarushwa.

Lakini utofauti wa jaribio hili ni kuwa, kombora halijarushwa kutoka ardhini, bali kwenye nyambizi chini ya bahari.
Kombora hili kuwa na uwezo wa kurushwa kutoka majini ni umuhimu zaidi kwa nchi hiyo kwa kuwa sasa wanauwezo wa kufanya mashambulizi mbali ya eneo lao.

Kwa mujibu wa maofisa wa Korea Kusini, kombora hili lina uwezo wa kuruka kwa kasi ya km 450 na kufika urefu wa km.910 kabla alijashuka baharini.

Hii ina maanisha kuwa makombora haya yana uwezo wa kuruka umbali mrefu mara mbili wa kiwango cha kimataifa ingawa makombora ya awali ya Korea Kaskazini yalikuwa na uwezo wa kuruka mbali zaidi.

Kwa mujibu wa BBC, Kombora hilo liliangukia baharini upande wa Japani, unaoitwa upande wa mashariki wa bahari. Japani imedai kuwa kombora hilo limetua katika umbali wa kilimita 200 kutoka ardhi yake.

Jaribio hilo linakuja muda mfupi baada ya Korea Kusini kusema kuwa mazungumzo ya nyuklia kati yao na Marekani yataendelea.

What appears to be a submarine-launched ballistic missile (SLBM) flies in an undisclosed location in this undated picture released by North Korea's official news agency

Nini kinafahamika kuhusu makombora hayo

Makombora hayo yalizinduliwa baharini siku ya Jumatano majira ya saa saba usiku saa za Afrika mashiriki, kilomita 17 kaskazini mashariki mwa fukwe za mji wa Wonsan .Ripoti kutoka televisheni ya taifa hilo KCNA imesema kuwa leo Alhamisi, majaribio matatu kutoka juu yatarushwa ,” makombora haya yamebuniwa kutoa vitisho kwa mataifa mengine na kujilinda”.

KNCA imeongeza kuwa hakuna madhara yatayotokea kwa nchi za jirani. Tofauti na majaribio ya awali hakukuwa na picha ya rais Kim Jong-un katika uzinduzi Katika majaribio kumi ya awali ya kurusha makombora mwaka huu, ni makombora la masafa mafupi tu ndio yaliorushwa.

Kama makombora hayo yalizinduliwa kwa kiwango cha kawaida, basi yale yaliyorushwa kwa kunyooka wima yana uwezo wa kusafiri kwa karibu kilomita 1900.

Hivyo masafa hayo yanaweza kuzifikia Japani na Korea Kusini. Lakini suala la makombora hayo kuzinduliwa majini, yanaweza kufanya makombora hayo kuwa na wakati mgumu kufanya kazi na kuziruhusu kufikia maeneo mengine walioyalenga.

Korea Kaskazini ina nyambizi iitwayo ‘Romeo’ kilijengwa mwaka 1990, na wanaamini kuwa na kasi ya kilomita 7,000

Nyambizi hiyo ina uwezo wa kufanya safari ya moja kwa moja mpaka kufikia Hawaii, Marekani. Chombo hicho cha majini kinachotumia nguvu ya mafuta ya dizeli, hata hivyo kinapiga kelele ambazo zinaweza kurahisisha kugundulika kirahisi.

Kuzinduliwa kwa kombora hilo la majini na Korea Kaskazini ni hatua mbaya zaidi kwa usalama wa majirani zake wa ukanda wa kaskazini mashariki mwa Asia.

Kombora hili limezinduliwa kwa mipango ya baadae ya majini lakini uzinduzi huu hauoneshi hilo. Wataalamu waliounda kombora hilo Korea Kaskazini wanasema kuwa ni hatari sana kufanya operesheni hiyo ya jaribio la kurusha kombora majini.

Ingawa kurushwa kwake kunaonekana kuwa ni mafanikio makubwa. Kama kombora hilo lingerushwa kama kawaida, yangeweza kufika katika visiwa vikubwa vinne vya Japan na ukanda wote wa Korea Kusini. Hii inatajwa kuwa mfumo hatari zaidi wa teknolojia ya kombora kutambulishwa katika taifa hilo.

Kabla ya jaribio la kurushwa kwa kombora hilo, Korea Kaskazini na Marekani zilithibitisha kuwa inajiandaa kufanya mazungumzo kuhusu nyuklia ndani ya wiki hii. Ingawa hakuna uhakika kama mazungumzo hayo yataendela

Marekani ilikuwa na lengo la kutaka taifa hilo kusitisha matumizi ya nyuklia. Majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yalianzia kwenye mkutano wa Hanoi, kati ya rais Donald Trump na Kim mwezi Februari bila ya kufikia makubaliano.

Wataalamu wanasema kuwa jaribio hilo kufanyika na kutangaza kwa mazungumzo hayo kuendelea kunaweza kuibua mgogoro.

Graphic showing a range of missiles built by North Korea

Mchoro huu hauoneshi kama kombora la ‘Pukguksong-3’, lina uwezo wa kuruka kwa kilomita 1,900

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents