Michezo

Kuhusu Aguero mimi siyo daktari – Pep Guardiola

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amezungumza na waandishi wa habari leo mchana kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea hapo kesho siku ya Jumamosi.

Meneja huyo wa City, Guardiola amegusia pia hali ya baadhi ya wachezaji wake ambao wanasumbuliwa na majeraha.

“Benjamin Mendy bado anaendelea huko Barcelona na atakuwa nnje ya uwanja hadi nusu fainali ya UEFA Champions League.”

Guardiola ameongeza “Aguero amepata ajali huko Amsterdam na atarejea hivi punde. Mimi sio daktari, atarejea na atapata hauweni”.

“Bado sijazungumza na Aguero nimefanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu. Nitazungumza naye leo”.

Gari lililohusishwa na ajali ya mchezaji wa City, Aguero

“Leo ni siku ya mapumziko na hivyo tunafuraha mimi ni mwalimu ambaye sipendi kufundisha kila siku kwasababu wanahitaji mapumziko kimwili na kiakili”.

Aguero apata ajali mbaya ya gari Uholanzi

 Kocha huyo wa zamani wa FC Bayern Munich amesema beki wa timu hiyo hatocheza.

“Kompany haja fanya mazoezi na sisi kwa msimu mmoja atakwenda kukutana na daktari wa Ubelgiji na kisha atarejea.Tutakuwa na mapumziko baada ya mchezo wetu na Chelsea na muda huu pia hatuwezi kuzungumzia kusajili nafasi ya beki wa kushoto”.

Guardiola amesema hawezi kutafuta mbadala wa Benjamin Mendy kwakuwa ni mchezaji mwenye uwezo na wakipekee kwa sasa duniani, wakati huo huo amewasifia wapinzani wake Chelsea kuwa na mchezo mzuri wa kushtukiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents