Michezo

Aguero apata ajali mbaya ya gari Uholanzi

Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Leonel “Kun” Aguero amepata ajali ya gari katika Jiji la Amsterdam huko nchini Uholanzi hapo jana siku ya Alhamisi.

Kun Aguero, amepata majeraha katika ajali hiyo masaa machache baada ya kuwasili katika tamasha la mwanamuziki raia wa Colombia, Juan Luis Londono Arias maarufu kama ‘Maluma’ lililokuwa linafanyika katika Jiji hilo kubwa la kifalme huku likijizoelea umaarufu kibiashara la Amsterdam.

Inaripotiwa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 29, alikuwa katika taksi akielekea uwanja wa ndege baada ya kutoka kumshuhudia msanii Maluma akitumbwiza .

Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Leonel “Kun” Aguero

Klabu hiyo imeripoti kuwa “Alikuwa nchini Uholanzi ikiwa ni siku yake ya mapumziko ndipo alipo pata ajali.”

Aguero anatarajiwa kuwasili Manchester leo siku ya Ijumaa nakufanyiwa vipimo vya afya kabla ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Chelsea siku ya Jumamosi.

Polisi wa Jiji la Amsterdam wamethibitisha kuwepo na watu wawili katika ajali hiyo ya taksi iliyotokea katika eneo la De Boelelaan.

Mapema mchana kabla ya ajali hiyo kutokea mshambuliaji huyo wa Argentina aliposti picha inayomuonyesha akiwa pamoja na msanii Maluma na kuandika ujumbe unaosema “ahsante kwa mualiko”.

Kun Aguero (kushoto) akiwa na msanii Maluma

Mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao saba katika michezo nane aliyocheza msimu huu na kumsaidia kocha wake, Pep Guardiola kuwa katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi ya Uingereza na kushinda michezo ya Klabu bingwa barani Ulaya

Kumekuwa na maswali mengi juu ya Aguero kile kilichompeleka nchini Uholanzi ilhali timu yake inamchezo mgumu na muhimu dhidi ya Chelsea siku ya Jumamosi.

Hivyo leo Kocha, Pep Guardiola atakuwa na mkutano na waandishi wa Habari hivyo hayo yatakuwa miongoni mwa maswali ambayo watu watataka kujua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents