Burudani

Kuimba ni vigumu kuliko kurap – Mandojo

Muimbaji Mandojo amesema wasanii wa Hip Hop wasiwabeze wasanii wa kuimba kwani muziki wa kuimba ni mgumu kuliko wa kuchana.

Mandojo

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Mandojo alisema kuchana kila mtu anaweza kuchana tofauti na muziki wa kuimba.

“Unajua kuimba inahitaji umakini zaidi kuliko kuchana,” alisema “Yaani kiukweli kabisa muziki wa kuimba ni muziki mgumu kuliko wa kuchana. Unajua kuchana mtu yoyote anaweza akachana lakini kuimba inahitaji kipaji fulani zaidi. Kuna watu wengi wanatamani kuimba lakini wanashindwa,” alisema Mandojo.

Mandojo na Domokaya ni miongoni mwa wasanii wa kuimba waliofanya vizuri sana katika kipindi cha nyuma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents