Habari

Kwa mara ya kwanza taifa la Uganda limerejelesha safari za ndege za kimataifa baada ya Corona kuzuia

Uganda imefungua tena mipaka yake ya kimataifa kwa mara ya kwanza tangu Machi, baada ya kufungwa kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Kufuatia hatua hiyo Shirika la ndege la Uganda imefanya safari ya kimataifa mapema Alhamisi kwa kutua katika mjini Nairobi na Mogadishu kama ilivyopangwa.

Ndege zingine za kimataifa pia zimetua nchini Uganda na pia kuanza safari.

Mamlaka ya usafiri wa anga imetoa wito kwa wasafiri kufika katika uwanja wa ndege saa nne kabla ya safari zao.

Maafisa wa uhamiaji katika uwanja wa ndege wamewashauri wasafiri kutumia kufuata maagizo waliyopewa ili kudhibiti hali ya watu kukaribiana

Kwa mujibu wa BBC. Wazara ya Afya imesema wasafiri wanaozuru Uganda watatakiwa kuwasilisha cheti cha kuonesha wamefanyiwa uchunguzi wa corona katika kipindi cha saa 72 kabla ya kuanza safari na kwamba hawana virusivya corona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents