HabariMichezo

Ladaki Chasambi alikataa shule kisa mpira

Ladaki Chasambi kijana mdogo mwenye kipaji kikubwa kutoka Kisaki mkoani Morogoro ambaye amepandishwa katika timu ya wakubwa ya Mtibwa Sugar rasmi msimu huu lakini akipewa nafasi Tangu mechi za msimu uliopita chini ya kocha Mayanga nankuonesha uwezo mkubwa.

Katika mchezo wa Leo kati ya Mtibwa Sugar na Mnyama Simba SC mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara watu wengi wamefutiwa na uwezo mkubwa na kiwango Bora Cha kijana mdogo kutoka U20 Ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji Bora wa vichuano ya vijana Tena mara mbili mfululizo (MVP) .

Ladaki Chasambi wamempandisha katika umri sahihi bwana mdogo katika mchezo wa Leo mbele ya Simba amefanya vitu vya msingi vya kuisaidia timu yake kucheza mpira pamoja na kupata magoli angalau mawili uwezo wake mkubwa wa kufanya Dribbling pamoja na kupiga accuracy pass kwenda kwa mlengwa ana maarifa nguvu pamoja na kasi ya Hali ya juu.

Chasambi bwana mdogo aliamini katika Mpira ndiyo ndoto yake alikataa shule mbele ya mzazi wake kuwa hataki shule anataka kucheza mpira ndiyo kitu anachokipenda na kukiweza,Ladaki amesoma form one pekee katika shule ya Morogoro Secondary.

Baada ya kukataa shule akajiunga na kituo Cha Moro kids Mungu akamshikia akachaguliwa kujiunga na Serengeti Boys ya KinaKelvin John akiwa mdogo walivyooka wakina Mbape akabaki yeye ndiyo nahodha wa timu ya Serengeti,Bwana mdogo sasa hivi anacheza ligi kuu soka Tanzania bara na anakiwasha.

NB:Keep Moving Chasambi ulikataa shule,Kisa Mpira inabidi utimize malengo yako.

By Issaya Dede

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents