Burudani

Lamar azisifia Tuzo za Kili 2011

lamar

Produza mahiri wa Muziki hapa nchini Lamar anayemiliki studio ya Fishcrab, amesema ana imani kubwa na tuzo za Kill Music Awards za Mwaka huu tofauti na miaka mingine iliyopita.

Lamar amesema ataendelea kufanya kazi zake kwa ubora ule ule kama ilivyo kawaida yake na kwamba hatokubali kuona anarudi nyuma katika utayarishaji wake wa Muziki kwa wasanii wote watakaohitaji kufanya kazi zao an yeye.

Lamar pia alisema tofauti na matarajio ya wengi kuhusu tuzo za Kill Music Awards, yeye binafsi ana amini kuwa tuzo hizo zimeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu hivyo kupelekea yeye kuwa na imani nayo.

Alisema kimsingi Kampuni ya bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro wamefanya kitu kikubwa kwa kuwawezesha watanzania kuwachagua wanamuziki wenye uwezo hasa wanaowaona ili kuwawezesha kupata tuzo hizo.

Alisema anafurahishwa na ujio wa tuzo hizo kwa mwaka huu huku akiamini kuwa lengo lake ni kuwapata wanamuziki bora na siyo bora wanamuziki katika kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents