Burudani

Zola adai kupiga Ndondi na Muziki

zola

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Zola D, amesema ataendelea kupigana kama kawaida  pamoja na kufanya muziki kwa kuwa mchezo huo unalipa kama ilivyo kwa michezo mingine.

Zola alisema tofauti na watu wanavyouchukulia mchezo wa ngumi , kwake binafsi mchezo huo anauzimia na kwamba ana imani kuwa ataendelea kufanya vizuri kila atakapopanda jukwaani kupigana.

Alisema watu wengi wamesema kuwa amevamia mchezo huo lakini yeye anadai kuwa mchezo huo ni kitu kilichokuwa moyoni mwake kwa kipindi kirefu hivyo watarajie mambo mazuri kutoka kwake kila atakapopanda ulingoni kwa ndondi.

Zola alisema hivi karibuni alipanda ulingoni kupigana na akaibuka na matokeo mazuri ikiwa ni katika kuwahakikishia wapenzi wa mchezo huo kuwa yupo fiti pia katika upande huo kama ilivyo kwa upande wa muziki.

Aidha ukiacha nyimbo yake aliyoifanya akimshirikisha Mangwea, hivi sasa yupo katika hatua za mwisho kufyatua albamu yake aliyoimwaga sifa katika kurasa za Bongo5 kuwa imekwenda shule tofauti na matarajio yake.

Amewataka watanzania na zaidi wapenzi wake kukaa mkao wa kuifaidi albamu hiyo pindi itakapokuwa hewani itakapokamilika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents