Habari

Licha ya mshahara wake kushuka, David Beckham ang’ang’ania Marekani

Mcheza soka wa nchini Uingereza David Beckham amekubali mshahara wake kupungua kwa paundi milioni
1.6 ili kuendelea kuishi Los Angeles, Marekani.

Kipindi nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza anajiunga na LA Galaxy mwaka 2007, alisaini mkataba wa miaka mitano ambao ulimpa kiasi cha paundi milioni 4.1 kwa mwaka.

Lakini kutokana na makubaliano katika mkataba wake mpya aliousaini mapema mwaka jana, Beckham mwenye umri wa miaka 37 atakuwa akilipwa paundi milioni 2.5.

Hata hivyo nyota huyo amekuwa na deals kadhaa za matangazo zikiwemo za perfume na nguo za ndani ambazo zinampa kiasi cha paundi milioni 160.

Kutokana na uamuzi wake wa kuendelea kuishi Marekani, sasa mchezaji huyo amepoteza nafasi yake kama mcheza soka wa Marekani anayelipwa pesa nyingi zaidi.


Nafasi hiyo sasa inashikiliwa na mfaransa Thierry Henry ambaye hupokea paundi milioni 3.5 kwa mwaka kwa kuicheza timu ya soka ya New York Red Bulls.

Beckham alikuwa amefikiria kuondoka LA Galaxy mwishoni mwa msimu uliopita lakini aliamua kubaki licha ya kupewa ofa kutoka kwa timu za Spurs, Queens Park Rangers na Paris Saint-Germain.

Akizungumzia uamuzi wake, Beckham mwenye watoto wanne alisema:“‘Mfumo wa maisha yangu ndo sababu. Familia yangu imepapenda hapa na watoto wametulia. Kuishi pembezoni mwa ufukwe ni raha. Umekuwa ni wakati mzuri sana uwanjani na nje ya uwanja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents