Burudani
Lil Wayne atolewa ICU
Baada ya kukaa kwa takriban siku 6, hatimaye Lil Wayne ametolewa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwenye hospitali aliyolazwa ya Cedars-Sinai jijini Los Angeles baada ya madaktari kuona kuwa afya yake imekaa vizuri kiasi.
Vyanzo vilivyo karibu na Weezy vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa kwa sasa Lil Wayne yupo kwenye chumba cha kawaida kwenye hospitali hiyo na hahitaji tena uangalizi wa karibu kama awali baada ya kuoverdose madawa ya kupunguza maumivu wiki iliyopita.
Lil Wayne amekaa ICU tangu Jumatano ya wiki iliyopita.Kwa sasa Lil Tunechi mwenye miaka 30 anasemekana kutembea mwenyewe lakini akiwa amezungukwa na timu ya mabodyguard. Pia anakula mwenyewe na anaweza kuruhusiwa hospitalini hapo siku chache zijazo.