Burudani

Linah ana collabo mbili za kimataifa kibindoni

Linah Sanga amesema tayari ameshafanya collabo mbili na wasanii wa kimataifa na amepanga kuzitoa mwakani.

12298833_944662165599178_1629279455_n

Ameiambia Bongo5 kuwa kazi hizo zitatoka mwakani kutokana na muda uliobaki kila msanii kutaka kutoa wimbo.

“Kabla sijafunga mwaka nilikuwa nataka kufanya kolabo kubwa za kimataifa. Nashukuru tayari nimefanikiwa ila siwezi kuziweka wazi nimefanya na nani na nchi gani.

Lakini ni kubwa na nimeshindwa kuziachia kwa sasa kutokana na muda uliobaki. Ila mashabiki wangu sitawaacha hivyo hivyo, kuna kazi mpya inaitwa Nia Yangu itatoka pamoja na video na baada ya hapo mwakani watu wakae mkao wa kula.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents