Michezo
Liverpool vs Man United kukutana kwenye fainali ya International Champions Cup
Mahasimu katika ligi kuu ya Uingereza, Liverpool na Manchester United wanakutana leo katika fainali ya International Champions Cup mjini Miami.
kikosi cha Van Gaal kikijianda na mechi ya leo dhidi ya Liverpool
Liverpool wameingia katika hatua hiyo ya fainali baada ya kuifunga Ac Milan 2-0 katika hatua ya nusu fainali huku Man United wakiifunga Madrid magoli 3-1 nakuingia fainali.
Wachezaji wa The Reds ‘wakipasha’ kabla ya mechi ya leo dhidi ya Manchester United
Mara ya mwisho watani hawa wajadi walikutana na Liverpool walishinda magoli 3-0 dhidi ya Man United katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu. Hii ni mara ya kwanza kwa makocha Brendan Rodgers na Van Gaal kukutana kabla ya ligi kuu ya Uingereza kuanza tarehe 16 August.