Habari

Lugola aonya tabia ya watuhumiwa kunyimwa dhamana na polisi ‘hii tabia ife haraka’

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola nchini Tanzania amewataka polisi kukoma kuwanyima watuhumiwa kunyimwa dhamana hasa siku za mapumziko, kwa kisingizio kuwa si siku za kazi.

Waziri huyo alisema hilo ni kinyume cha sheria na mtu yeyote anayestahiki kupewa dhamana anafaa kuhudumiwa katika chini ya saa 24 wakati wowote ule.

Bw Lugola alisema hayo katika kijiji cha Busanza wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jumapili.

“Hii tabia sijui imetoka wapi na imejengeka kwa baadhi ya askari polisi. Eti mtu akiingia mahabusu siku ya Ijumaa ikifika Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

Waziri huyo alisema vituo vya polisi nchini humo huwa vinafanya kazi siku zote za wiki zikiwemo za mapumziko na haoni ni sababu gani inayoweza kuwafanya polisi kutompa mtuhumiwa dhamana.

Aliahidi kuchukua hatua dhidi ya askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana.

Kwa mujibu wa waziri huyo, dhamana ni haki ya mtu endapo kosa lake linadhaminika.

Aidha, aliwataka huku akiwataka wananchi watakaoombwa fedha ili wapewe dhamana kuripoti tukio hilo kwa maofisa wa ngazi za juu ili askari husika achukuliwe hatua za kinidhamu.

“Kuna tabia iliyozoeleka katika jamii, eti kuingia polisi ni bure ila kutoka ni fedha, hii kauli nataka ife kwa sababu nawajua polisi na hawanidanganyi kwa lolote,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents