Burudani

Mabeste asimama kufanya muziki kwa muda kumuuguza mke wake

Rapper Mabeste ametangaza kusimama kufanya muziki kwa muda ili kupata nafasi ya kumuuguza mke wake.

mabeste4

Mabeste amesema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya kuachia wimbo ‘Bubu.

“Ndugu zangu naomba mtaniwia radhi, nilidhani nitakua sawa tayari kwa kaz za mzik wangu mwaka huu! Lakini imekua tofauti na nilivyo
fikiria,” ameandika Mabeste kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Hali ya mke wangu imejirudia hali yake c nzuri tena c mtu wa kuachwa peke yake mda wote natakiwa niwe nae karibu hivyo inanilazimu kusimama kazi zangu za mziki kwa sasa mpaka pale Mungu atakapo barikia hali yake kurudi kama zamani,” ameongeza.

“Mniwie radhi fans wangu maana najua mlinimiss! Kwa vile najua mnampenda mabeste bas naomba endeleeni ku support USIWE BUBU hapo ndo mtaendelea kumskia mabeste mpaka pale atakapo maliza kipindi hiki kigumu Mungu atakapo penda! Ilikua niachie usiwe bubu video mwez huu wa pili ila haitawezekana tena! Mniwie radhi nawapenda sana.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents