Burudani

Madee amchana Dudu Baya, ‘hatusikii kazi tunasikia maneno’

Msanii wa muziki Bongo, Madee amemjibu msanii Dudu Baya aliyedai kuwa wimbo ‘Sikila’ si mzuri.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sema’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anachukulia hayo ni kama maoni yake binafsi kwani hakuna ambaye anafanya kitu bila kupingwa na msanii hawezi kutoa ngoma kila mtu akaikubali.

“Hatusikii kazi tunasikia maneno, kwa hiyo hivyo ni vitu ambayo kwangu mimi huwa navipisha tu, ukitaka kubishana nakuonyesha kazi yangu hii hapa, nadhani huo ndio msingi bora ambao tunatakiwa tuwaelekeze wezentu wanaojaribu kutoka nje ya mistari,” amesema Madee.

“Wengi ambao nilikuwa nao, nilianza nao miaka hiyo 17 ndio ambao sasa hatuwasiki zaidi utawasikia wanaongea hiki na kile lakini still Madee bado anatoa ngoma watu wanapokea na show zinafanyika na maisha yanaendelea vizuri tu,” amesema.

Ngoma Sikila ambayo Madee amemshirikisha Tekno kutoka nchini Nigeria alifanya video katika mtindo wa katuni (animation) kitu ambacho Dudu Baya alieleza kuwa hakiendani na Madee aliyemfahamu hapo awali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents