Michezo

Ronald Koeman ahofia kukumbwa na jinamizi la Ancelotti

Klabu ya Everton inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa imetoshana nguvu ya mabao 2-2 dhidi ya Apollon Limassol katika michuano ya Uefa Europa League iliyoendelea hapo jana usiku hatua ya makundi.

Meneja wa klabu hiyo, Ronald Koeman

Meneja wa klabu hiyo, Ronald Koeman amesema lengo kubwa katika mchezo wao ilikuwa nikupata ushindi na wala siyo suluhu kama waliyopata.

“Mawazo yetu yalikuwa ni kupata ushindi leo na wala sio suluhu kweli wameniangusha. Tulianza mchezo tukiwa wadhaifu ambao tumekosa kujiamini na kujikuta tunafanya makosa ya hapa na pale.” Amesema Koeman.

“Kipindi chapili kilikuwa kizuri zaidi kwetu kwakuwa tuliweza kuumiliki mchezo na kupata nafasi nyingi za kushinda bao la tatu lakini huo ndiyo mpira wakati mwingine kadri una vyopambana kufunga ndivyo unavyopata hofu ya kucheza ukiwa huru.”

“Siwezi kusema vijana wangu hawaja pambana lakini naweza kusema walikuwa na hofu zaidi ya kushambulia.”

Mabao ya timu hiyo yakifungwa na Rooney dakika ya 21 kipindi cha kwanza na mchezaji, Nikola Vlasic dakika ya 66 mchezo.

The Toffees wana pointi moja katika michezo miwili waliyoshuka dimbani mpaka sasa.

Na Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 wakiwa ugenini walipocheza dhidi ya Bate Borisov mchezo wa kundi H

Katika michezo mingine Ac Millan imeshinda 3-2 dhidi ya Rijea, Lyon pia wamefanikiwa kutoa sare na Atlanta baada ya kufungana bao 1-1.

FC Cologne imefungwa bao 1-0 na FK Crvena Zvezda, Salzburg imeshinda bao 1-0 dhidi ya Marseille, Oestersunds FK imeichapa Hertha Berlin bao 1-0, Konyaspor imetakata kwa ushindi wa bao 2-1 na Vitoria de Guimaraes.

AEK Athens imetoshana nguvu na Austria Wien ya bao kwa kufungana bao 2-2. Nice imeichapa Vitese mabao 3-0, Mainz imekubali kipigo cha bao 1-0  dhidi ya Hoffeinheim, Partizan imechapwa na Dynamo magoli 3-2 na Maccab Tel Aviv imetoka sare na Villareal 0-0. Fc Sheriff imetoshana nguvu ya kutofungana na klabu ya Koeben

Lugan imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya FC FCSB ,Plesen imeichakaza Hapoel bao 3-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents