Habari

Madiwani 46 wa Chadema waliohamia CCM wamuibua Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe amesem madiwani 46 wa chama hicho waliojiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakuwezi kuiua Chadema.

Mbowe amesema madiwani wa Chadema nchi nzima wapo zaidi ya 1,130, hivyo madiwani 46 waliohama na kwenda ni kitendo kinachowapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli wanaweza kukisimamia chama.

“Kazi kubwa inayofanywa na CCM ni kuwakatisha tamaa na jambo ambalo limefanyika karibuni ambalo linaonekana wana Chadema wengi wamerudishwa nyuma basi ni suala la madiwani,” amesema.

“Hiki chama hakifi mzee, Chadema nchi nzima ina madiwani 1,184 madiwani mpaka dakika hii wameondoka ni madiwani 46 kwa hiyo tuna madiwani zaidi ya 1130 wamebaki, halafu mtu anasema CHADEMA inakufa una akili wewe?” amesema Mbowe.

Aidha Mbowe amesema kuwa hao viongozi ambao wanahama kutoka Chadema na kwenda CCM kwao ni kama funzo kwamba wapo viongozi na watu mbalimbali ambao wapo ndani ya Chadema kwa lengo la kutafuta fursa za ulaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents