Habari

Maelfu ya watu waupokea mwili wa Dkt. Mengi Kilimanjaro, haijawahi kutokea mapokezi kama hayo (+Video)

Hatimaye wakazi wa Moshi na maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro leo Mei 8, 2019 wamejitokeza kwa wingi kuupokea mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi.

Mapokezi hayo yamehudhuriwa na maelfu ya waombolezaji waliokuwa wamekaa barabarani kuupokea nwili huo ulioagwa jana Jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo ya wenyeji wa mkoa huo wamesema haijawahi kutokea mapokezi makubwa kama hayo, ingawaje misiba mikubwa imewahi kutokea mkoani humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents