Habari

Wanasiasa wa upinzani wenye nguvu zaidi Uganda, Bobi Wine na Kizza Besigye waungana kumsambaratisha Rais Museveni

Mbunge wa upinzani nchini Uganda ambaye pia ni msanii wa muziki, Robert Kyagulanyi  maarufu kama Bobi Wine ameungana na mwanaharakati wa kisiasa Dkt. Kizza Besigye wameahidi kushirikiana kukiondoa madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.

Image result for bobi wine and kizza besigye
Kizza Besigye na Bobi Wine

Taarifa iliyotolewa na wawili wapinzani hao wenye nguvu zaidi nchini Uganda, imeeleza kuwa baada ya mazungumzo kati yao, wamekubaliana kuhusu masuala kadhaa wakati wanapokuja pamoja kushirikiana kisiasa dhidi ya rais Museveni kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2021.

Hapo jana akizungumza na waandishi habari, Bobi Wine alisema wamekuwa wakishauriana katika mikutano kadhaa na vyama tofuati vya kisiasa nchini kikiwemo cha Democratic Party maarufu DP bloc na hivi karibuni na kiongozi wa People’s government, Dkt Kizza Besigye.

Bobi yeye hana Chama ni mgombea huru na kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kyadondo, Na Chama tawala cha NRM kinachoongozwa na Rais Museveni kimekuwa madarakani tangu 1986.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents