Habari

Mafuta kuendelea kuzalishwa kwa kiwango cha chini duniani – OPEC+

Mataifa yenye nguvu kubwa katika uzalishaji wa mafuta duniani yanayoongozwa na Saudi Arabia na kwa upande mwingine Urusi yamehitimisha mkutano wao kwa kukubalina kudumisha viwango vyao vya sasa vya uzalishaji wa mafuta katika hali ya sintofahamu na ikiwa kabla ya kuanza kutekelezwa vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Moscow vyenye kutarajiwa kuanza juma hili.

Mataifa hayo 13 wanachama wa umoja wa OPEC wanaoongozwa na serikali ya Riyadh na washirika wao mataifa mengine 10 yenye kuongozwa na Urusi, kwa  ujumla wa mataifa 23 yakijulikana kama OPEC+ wameamua kuzingatia makubaliano ya Oktoba ya kupunguza uzalishaji wa mapipa milioni mbiili kwa siku hadi mwishoni mwa 2023.

Nafasi ya hatua za dharura zitakapohitajika

Lakini hata hivyo mataifa hayo, katika mkutano huo wamekubaliana kuchukua kukutana muda wowote kuanza sasa na kufanya mabadiliko yanayohitajika kwa kutegemea mahitaji ya soko.

Mchambuzi katika masuala ya nishati kutoka taasisi ijulikanayo kama ABN AMRO,Hans van Cleef  amesema uamuzi huo wa Jumapili ulitegemeewa sana  na kwamba hukuwa na la kushangaza,ikizingatiwa hali ya kudorora kwa uchumi, hatua ambayo imeshusha bei ya pipa la mafuta kufikia dola 90 pamoja na kupunguzwa huko kwa viwango vya uzaslishaji.

Muungano huo unaojulikanao kwa pamoja kama OPEC+, umesema uamuzi wake wa Oktoba wa kupunguza uzalishaji “ulisukumwa tu na hali juma la soko, na kuongeza kwamba umekuwa lazima kuwepo kwa njia ya lazima na sahiki katika kuleta hali tulivu katika soko kote duniani.

Punguzo la uzalishaji wa mafuta la Oktoba ni la kihistoria

Hatua ya upunguzaji wa uzalishaji mafuta ya  Oktoba kwa mataifa hayo yenye nguvu katika nishati hiyo inaakisi kiwango kikubwa zaidi cha punguzo  tangu kuongezeka kwa janga la Covid mwaka 2020, hatua iliyopingwa vikali la Marekani katika makabiliano yake na Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents