Habari

Mahakama kumkamata aliyempa Sabaya mili 90?

Hakimu wa Mahakama ya Mkazi Jijini Arusha, Dkt. Patricia Kisinda anatarajiwa kutoa uamuzi mdogo kuhusu ombi la kukamatwa kwa shahidi namba 10 Evarist Mrosso Disemba 6.

Dkt . Kisinda amesema hayo baada ya majibizano ya kisheria yaliyokuwepo mahakamani leo Disemba mbili ambapo Mawakili wa Jamhuri walikuwa wakipinga hoja zilizoibuliwa na utetezi ambapo mojawapo ikiwa ya kumkamata Shahidi Mrosso kwa kuwa amekiri mahakamani kutoa rushwa ya Milioni 90 kwa Lengai Ole Sabaya.

Awali, Disemba moja, mawakili wa Jamhuri waliomba kupatiwa wiki mbili ili kuwasiliana na mamlaka iliyowateua kusimamia kesi hiyo lakini siku ya leo, Hakimu Kisinda alipiga chini ombi hilo na kuwataka Jamhuri wajibu wao kwa kuwa ndio wapo mahakamani, na kuwapatia Saa mbili za kujiandaa kitu ambacho Jamhuri walisema hawahitaji na kwamba wanauwezo wa kujibu hoja hizo bila kupatiwa muda.

Wakianza kujibu hoja ya kwa nini Shahidi Mrosso mpaka leo hajakamatwa, Wakili Mwandamizi Felix Kwetukia alisema mwenye mamlaka ya kushitaki ni Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP), hivyo basi kwa mamlaka alonayo anauwezo wa kushtaki na kuamua nani awe shahidi. Hivyo mpaka leo Mrosso kutoshtakiwa ni suala la mwenye mashtaka DPP.

Akijibu hoja ya namna shahuri lilivyochunguzwa hadi kufika mahakamani, Wakili Tarsila Gervas amesema mwenye mamlaka ya kufanya upelelezi ni DCI hivyo yeye ndiye mwenye maamuzi ya shauri lifanyiwe upelelezi na nani kwani hata TAKUKURU waliochunguza faili hilo wapo chini ya DCI.

Na kuhusu ni Mawakili wa Serikali wanaosimamia kesi hiyo badala ya Mawakili kutoka TAKUKURU, Wakili Tarsila amesema kwamba DPP ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua wasaidizi wa kusimamia kesi, hivyo wao wako hapo kisheria kumuwakilisha DPP na kwamba Mkurugenzi huyo hawezi kuzunguka nchi nzima.

Pamoja na hoja hizo Wakili wa Utetezi, Edmund Ngemela amesema msingi mkubwa umejikita katika kifungu cha 17 cha sheria ya makosa ya jinai na kwwmba ni kifungu ambacho kinatoa muongozo wa namna gani makosa ya jinai yanapaswa kushughulikiwa.

Akaongeza kuwa Hakimu akiona yafaa anaweza kumkamata shahidi na kuwa haina haja ya kutumia nguvu nyingi bali mahakama iangalie na kuona inafaa kutenda vipi.

Sabaya na Wenzake sita wanashtakiwa kwa kosa la Uhujumu Uchumi ambapo wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi milioni 90 kwa ndg Evarist Mrosso Januari 22 2021.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents