January Makamba ahoji, Nani anamiliki rights za mechi kutangazwa ? Nani ana haki ya kuziuza?

Ameandika Mbunge huyo wa Bumbuli January Mkamba kuwa “Hizi TZS 300m anapewa nani? Swali la jumla: nani anamiliki rights za mechi kutangazwa? TFF, League Board, au timu? Nani ana haki ya kuziuza? Kama timu hazina rights, je zina nafasi kuamua nani anauziwa na kwa bei gani? Je, rights zinaweza kuuzwa match by match na sio Ligi nzima?.

Ikumbukwe mapema leo asubuhi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeingia mkataba wa miaka 10 na TFF wa kutangaza Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya TZS bilioni 3.5. Kwa mkataba huo, hakuna chombo cha habari kinachoruhusiwa kutangaza mpira wa miguu kwa njia ya sauti bila kuwa na makubaliano na TBC.

Related Articles

Back to top button