Habari

Makosa ambayo watu hufanya wanapotafuta marafiki wapya sehemu wasiyofahamika

Kama ndio kwanza umefika mji mpya kikazi au kibiashara ni jambo ambalo linakufanya ujiskie kama unapata hewa nzuri katika maisha ya watu wanaokuzunguka na hasa watu ambao wamekuwa marafiki zako wanabadilika hivyo unapata watu wapya wa kuzungumza nao , mazingira mapya na hata utamaduni mpya. Hivyo unahitaji watu wapya tofauti na kule ulikotoka, mara nyingi utajitahidi kupata marafiki wengi wenye mvuto kwako.

friends-talking

Lakini usifanye makosa ambayo watu wengi wamekuwa wakifanya wanapokutana na marafiki wapya au watu wapya

Watu hufanya makosa wanapofika sehemu ambayo hawafahamiki, wanafikiri wakienda klabu za pombe na sehemu za starehe ndipo watakutana na marafiki wapya. Hivyo watu wengi hujikuta wakienda sehemu ambazo hazina mahusiano na haiba zao, kumbuka wanaokutana klabu za pombe au sehemu nyingine za starehe ni wale ambao wamekuwa marafiki tayari hivyo wanakwenda kufurahi pamoja na sio kutafuta marafiki wapya. Urafiki unafanya kazi pale ambapo kuna kitu kitawaleta pamoja, kama kuna jambo kwenye jamii, watu wenye haiba yako, matukio muhimu ya kibiashara au kikazi au hata hafla rasmi.

Katika mazingira kama hayo ni rahisi kupata marafiki wapya au kukutana na watu wapya.

Kama unataka kupata marafiki wapya unahitaji kujiunga na jamii uliyoikuta. Tatizo hapo ni kwamba unahitaji wewe mwenyewe kushirikiana nao, hata kama ni kwa muda mrefu katika siku hiyo, unahitaji kutoka nyumbani kwako na kwenda kukutana na watu. Tafuta watu au marafiki wenye haiba yako na uanze kuongea nao kabla ya kujiunga nao, unatakiwa ujue wanafanya nini, madhumuni yao na kama yataendana na wewe au la!

Ingawa kuna ujuzi ambao utakufanya lazima ukutane na watu wapya unapokwenda mahali fulani na itakuwa sehemu ya maisha yako.

  • Hatua ya kwanza: Tafuta jamii ya watu wanaokuzunguka au karibu na unapoishi. Tunapozungumzia jamii ni watu wenye haiba au watu wanaoendana na wewe. Inaweza ikawa kama ni mchezaji wa mpira utakwenda uwanjani na sio klabuni, kama ni muumini wa dini utakwenda kule wenzako wanakokutana n.k .
  • Hatua ya Pili: Hudhuria matukio yao kama ni aina ya watu ambao ungependa kuwa marafiki zako.
  • Hatua ya Tatu: Nenda kwa mtu ambaye anaongoza hilo kundi, jitambulishe na waambie kama unapenda wanachokifanya na kama unaweza saidia kwa namna moja ama nyingine. Usitoe ahadi kubwa ila ahidi kufanya kulingana na muda ulionao.
  • Hatua ya Nne: Inawezekana watapendezwa na wewe na wakakuomba kufanya kitu. Unachotakiwa kufanya hudhuria matukio yao bila kukosa hasa yale ambayo umeahidi kufanya kitu, na usiahidi zaidi ya kile unachoweza kufanya.

Hebu ujue kwanini hizo hatua zinafanya kazi…………

  • Sababu ya Kwanza : Kama hutafanya uamuzi wa kukutana na watu , utakachokutana nacho ni watu ambao hukutarajia ndio wanakuwa marafiki zako bila sababu za msingi.
  • Sababu ya pili: Ukifuata utaratibu huo, watu watakuona kwenye jamii hiyo mpya kama mtu wenye thamani na ambaye anaweza kuleta mageuzi na masaada mkubwa kwa jamii hiyo kimawazo, kifikra na matokeo bora kwa watu. Utajijengea heshima na kupata marafiki ambao wana mtizamo kama wako kwa kuona kile unachofanya.
  • Sababu ya Tatu: Watu hupenda kujua nani anaongoza hilo tukio, watu watakuja kwako ili wakufahamu. Hutahitaji kutumia nguvu nyingi kwasababu watu watakuwa wamekuzunguka.
  • Sababu ya Nne: Ajabu ni hii hapa: inahitaji wewe kuondoka kwenye mazingira yako uliyoyazoea ili ukutatane na watu wapya. Kama utasaidia jamii uliyoikuta, utapata watu na wala hutahangaika kujua nani ni nani bali utajua wanaokuzunguka hivyo kufanya maamuzi sahihi.

Kwa mara ya kwanza kama utakutana na mtu mmoja katika tukio moja au wawili kama kuna matukio kila wiki unaweza kukuta umekatana na watu sita au saba na kuweka msingi na mtaji.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents