Burudani

Malengo yangu, Kuwa Msanii mkubwa kumzidi Diamond kimafanikio kwenye Muziki- Mr. Huba

Kwenye hii Dunia kila mmoja anamalengo yake na kuna watu wanawashawishi hadi kuwatia moyo kuendelea kupambana kufikia malengo yao.

Hii sio kwenye muziki tu, Bali karibia kwenye kila sekta kuna watu ambao wamefanikiwa na wanakuwa ni hamasa ya wengine kupambana ili kutoboa kwenye fani husika.

Mr. Huba ni moja ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye yeye amekuwa akitumia mafanikio ya msanii maarufu wa muziki hapa Tanzania, Diamond Platnumz kama chachu ya yeye kupambana zaidi kwenye muziki.

@mrhuba_ anasema ili ufanikiwe ni lazima uwe na wivu wa kimaendeleo na sio chuki kwa wale watu waliofanikiwa, Hiyo itakufanya upambane zaidi ikibidi uwazidi kimafanikio kama Diamond Platnumz alivyoanza muziki hadi leo namba moja Tanzania.

“Diamond alianza kama sisi watu walimchukulia poa, Yeye hakujali alikuwa na malengo yake makubwa na kweli akakaza tangu mwaka 2008 huko mpaka leo hajawahi kushuka kimuziki, Mimi naamini siku moja nitamfikia ikibidi hata kumzidi kimafanikio kwenye muziki” Amesema Mr. Huba akihojiwa na Bongo5.

Kwa upande mwingine, @mrhuba_ amesema Wasanii wengi wanaofanikiwa wanabweteka na mafanikio yao na kujikuta wanaanza kushuka na ndio maana Muziki wetu haukui kwa kasi kama Nigeria au Afrika Kusini.

“Ujue Tanzania wasanii wengi waliotoboa wanajisahau sana na kujiona wamefika Ila kiukweli bado Sana. Wenzetu Nigeria kila mwaka unakuta wasanii wapya wakubwa wanaongezeka ila hapa kwetu msanii akianza kupata jina tayari anaachana na muziki na kuanza Kiki kupata attention”.

Kuhusu malengo yake, Mr. Huba anasema kuwa anaamini atakuja kuwa msanii mkubwa Tanzania na pengine hata kumzidi Diamond Platnumz ambaye anamtazama kama kioo kwenye muziki hapa Nchini.

“Mimi naamini watu wote tunazaliwa sawa ila Juhudi, Nidhamu, Maarifa na Kumcha Mungu ndio ambavyo ukivizingatia utaongeza utofauti kwenye fani unayoifanya. Mimi naamini hivyo vimemfanya Diamond afike hapa alipo, Na mimi naamini katika hizo nguzo tatu na nazitii na kuziishi, Nitatimiza malengo yangu Inshallah” Amesema Mr. Huba.

Kwa mwaka huu Mr. Huba tayari ameachia kazi mbili moja kamshirikisha Kassim Mganga unaitwa ‘Laghai’ Bofya hapa chini kutazama;

Na mwingine mpya unaitwa ‘TIYARA’ Pia wiki hii anatarajia kuachia video ya wimbo huo, Ambao umepokelewa vizuri sana mitandaoni na kwenye Media tofauti tofauti.

Unaweza kucheki kazi zake nyingine kwa kubofya link iliyopo kwenye akaunti ya Instagram @mrhuba_ kutazama kazi zake zote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents