Habari

Mambo 13 yaliyojiri Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu

Mambo makuu 13 yaliyojiri bungeni katika kipindi cha maswali na mjibu leo Novemba 17 mwaka huu. Ambapo bunge hilo limeongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson.

Katika mkutano wa tisa kikao cha tisa wabunge mbalimbali waliuliza maswali na kujibiwa na serikali kama ilivyo kawaida, haya ni mambo 9 kwa ufupi yaliyozungumzwa ndani ya Bunge.

#Serikali imeendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo ya barabara za Halmashauri ili ziweze kupitika kwa kipindi chote. Mhe. Kandege

#Serikali imekuwa na utaratibu wa kuajiri wataalamu wa kada ya Afya kipindi wanapohitimu mafunzo na kufaulu vizuri katika masomo yao- Mhe. Kandege.

#Serikali inaendelea kuboresha mazingira kama vile upatikanaji wa nyumba pamoja na huduma za kijamii ili kuwafanya Watumishi wanaoajiriwa waweze kubaki katika maeneo yao waliyopangiwa- Mhe. Kandege

#Serikali ina mikakati mbalimbali ya kuboresha utoaji wa elimu nchini ikiwemo kutenga fedha za ujenzi wa nyumba za walimu- Mhe. Kandege

#Kuondoa VAT kwenye vifaa vya ujenzi kwa lengo ka kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za makazi kunaweza kabisa kuwanufaisha zaidi wafanyabiashara wachache kuliko wananchi wa kawaida, na pia kusababisha kupungua kwa mapato ya Serikali na hivyo Serikali kuwa na uwezo mdogo wa kutoa huduma muhimu kwa Umma- Dkt. Kijaji

# Lengo la kutoza kodi ni kuiwezesha Serikali kuwa na mapato ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa huduma muhimu za jamii kwa wananchi wote- Dkt. Kijaji

#Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya Uvuvi nchini kwa kutekeleza mikakati yenye lengo la kuendeleza wavuvi ili waweze kupata ajira, lishe, kipato na kuchangia katika pato la Taifa- Mhe. Ulega

#Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo inatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wakulima wakiwemo wavuvi na wafugaji ili waweze kununua zana bora za uvuvi- Mhe. Ulega

#Serikali imeondoa kodi kwenye zana na malighafi za uvuvi zikiwemo injini za kupachika, nyuzi za kushonea nyavu na vifungashio kupitia Sheria ya Ongezeko la Thamani( VAT) ya mwaka 2007- Mhe. Ulega

#Katika kukabiliana na tatizo la uchakavu na upungufu wa nyumba za kuishi Askari Polisi, Serikali inampango wa kujenga nyumba mpya katika jiji la Tanga na maeneo mengine kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha- Mhe. Nchemba

#Mipango ya Serikali ni kukiendeleza kiwanda cha Urafiki ili kizalishe nguo na mavazi ya aina mbalimbali- Mhe. Mwijage

#Shirika la Nyumba la Taifa linaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Miongozo ya Serikali- Mhe. Mabula.

#Serikali imeanza kutafuta fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa viwanja vya Ndege mbalimbali nchini- Mhe. Kwandikwa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents