Michezo

Manny Pacquiao awaomba radhi wanao jihusisha na uhusiano wa jinsia moja

Bondia Manny Pacquiao imembidi kuomba radhi kutokana na upinzani mkubwa alioupata kutoka kwa wale wanaounga mkono uhusiano ya jinsia moja.

Manny-Pacquiao-causes-outrage-for-his-shocking-statement-against-gay-marriage

Kumezuka upinzani pale ambapo Pacquaio ambaye pia ni mbunge huko kwao ufilipino aliposema kupitia televisheni kuwa matendo ya jinsia moja ni mabaya kuliko ya wanyama.

Pacquiao alisema, “kwa akili ya kawaida hata wanyama wanajua huyu dume huyu jike, mnyama dume hampandi mnyama dume na jike hampandi mnyama jike, kwa hivyo wanadamu tukiruhusu uhusiano wa jinsia moja basi tunafanya matendo mabaya kuliko hata hao wanyama”.

Watu walipomzonga sana, akaweka mtandaoni , picha yake akiwa na mkewe, sasa wamemzonga zaidi kawaomba msamaha lakini akawaambia nimeusema ukweli kama ulivyo kwenye misahafu, Mungu awabariki na ninawaombea.

BBC walitoa hii taarifa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents