Habari

Marekani hatarini kuishiwa fedha

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametahadharisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuishiwa fedha mwezi ujao na amelitaka bunge la nchi hiyo liongeze uwezo wa serikali wa kukopa.

Waziri Yellen ametoa tahadahri hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Nancy Pelosi. Katika barua hiyo waziri huyo amesema ikiwa bunge halitaongeza kima cha mikopo, serikali ya Marekani itaishiwa fedha mwezi ujao wa Oktoba na kwamba kwa mara ya kwanza katika historia yake Marekani haitakuwa na uwezo wa kutimiza dhima zake za kifedha.

Deni la serikali ya Marekani liliongezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa janga la COVID-19 baada ya serikali hiyo kupitisha mipango mitatu ya matumizi makubwa ili kupunguza athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents