Marekani inataka vita baridi – China

Balozi wa China nchini Uingereza amesema kuwa Marekani inajaribu kuanzisha vita baridi mpya na taifa hilo la kikomunisti kwa sababu inatafuta kisingizio kuelekea uchaguzi wa Rais mwezi Novemba.

Ambassador Liu Xiaoming in a signed article for The Daily ...

Balozi huyo Liu Xiaoming, amesema siyo nchi yake iliyogeuka mbabe bali ni upande wa pili wa bahari ya Pacific unaotaka kuanzisha vita mpya baridi dhidi ya China, na hivyo wanalazimika kujibu hilo.

Balozi huyo aliezungumza na waandishi wa habari, ameongeza kuwa China haina maslahi yoyote katika vita baridi na wala haitaki vita vyovyote.

Amesema wameona kila kinachoendelea nchini Marekani, wakitaka kuitumia China kama kisingizio na kuilaumu kwa matatizo yao na kwamba wanajua hii ni kwa sababu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi.

Related Articles

Back to top button