Habari

Marekani yazipa siku 60 kampuni zinazoshiriki mradi wa nyuklia Iran

Serikali ya Marekani imeweka ukomo kwenye mpango maalumu ulioziruhusu kampuni za Ulaya, Urusi na China kushiriki katika mradi wa nyuklia wa Iran.

USA Has Beaten Coronavirus, Declares Donald Trump | The Weather ...

Kampuni hizo sasa zimepewa muda wa siku 60 kuwa zimehitimisha shughuli zao nchini Iran. Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliyeitangaza hatua hiyo ametaka muda kwa kampuni zinazoshirikiana na kinu cha nyuklia cha Bushehr kupewa muda wa hadi siku 90 kuwa zimeondoka huko.

Utawala wa Rais Donald Trump unafuata sera ya shinikizo kali dhidi ya Iran, kama mkakati wa kuwalazimisha viongozi wa Tehran kukubali mkataba mpya kuhusu mpango wake wa nyuklia ambao utakuwa na masharti magumu zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents