HabariMichezo

Mashabiki wa PSG hawamtaki Messi, wafurika nje ya uwanja na kushinikiza aondoke

Hadithi ya PSG na mshindi wa Kombe la Dunia na nahodha wa Argentina Lionel Lapuga Messi inaweza ikawa ndio mwisho wake.

Sio tu mashabiki hawamtaki bali vyanzo vya karibu ya Messi viliripoti kuwa Messi hataki pia kuendelea kusalia jijini Paris.

Huenda Messi akajiunga na moja ya klabu kutoka Saudi Arabia au akarudi Barcelona, moja ya klabu inayotajwa sana Saudi Arabia ni Al Hilal na inaelezwa alienda Saudi Arabia kwa ajili ya mazungumzo.

Siku ya juzi jumanne alifungiwa wiki mbili na klabu hiyo baada ya kujiamulia kwenda Saudi Arabia bila ruhusa ya timu yake.

Baadaye siku ya jumatano taarifa zikatoka kuwa Messi habaki tena PSG, mashabiki wakaona usituchezee wewe, wakaamua kwenda nje ya uwanja wa PSG na kuamza kuimbi Messi hatukutaki.

Messi ni mchezi pekee aliyepata mapokezi makubwa Paris baada ya kuondoka Barcelona.

Shida iko wapi kwa Messi na Ronaldo?? Siku kadhaa nyuma pia imeripotiwa Ronaldo hataki kuendelea kubaki Al Nassr.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents