Habari

Matokeo ya darasa la saba yatangazwa 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu, ambapo watahiniwa zaidi ya milioni 1.07 kati ya zaidi ya milioni 1.34 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.

Kati ya hao wasichana ni 558,825 na wavulana ni 514,577.

Akitangaza matokeo hayo mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Almasi amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97.

Amesema kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents