HabariMichezo

Suarez akataa kuiomba radhi Ghana kwa goli lake la mkono World Cup 2010

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez amesema kuwa kamwe hawezi kuomba radhi kwa Ghana kutokana na kitendo chake cha kufunga goli kwa mkono katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

Suarez amesema angeomba radhi kama tu, angemjeruhi mchezaji lakini Ghana wenyewe walipata mkwaju wa penati na mchezaji wao akakosa.

Nakuongeza kuwa alisherehekea kitendo cha Ghana kukosa penati kama vile wamefunga goli.

Nyota huyo amesema hayo wakati timu yake ya Uruguay ikijiandaa kukabiliana tena na Ghana hapo kesho kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents