Habari

Mawakili kesi ya Sabaya waweka pingamizi nyaraka za ushahidi zisipokelewe, mahakama kuamua leo

Mawakili wa upande wa Utetezi, katika Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake Sita wameweka pingamizi la kupokelewa kwa ushahidi ambazo ni nyaraka za Benki kutoka tawi la kwa Mromboo, Arusha.

Wakili Mosses Mahuna akiteta jambo na washtakiwa

Akiweka pingamizi hilo, ambalo limeungwa mkono na Mawakili wengine, Wakili wa mshtakiwa namba moja na namba mbili, Mosses Mahuna amesema kwamba nyaraka hizo hazijakidhi vigezo kulingana na sheria ya ushahidi.

Mbali na kuvitaja vifungu vya sheria, Mahuna amesema Wakili wa Serikali ndiye aliyeomba mahakama ipokee nyaraka hizo kutoka benki ya CRDB kwa Mromboo, na siyo shahidi ambapo amezitaja nyaraka hizo ni , bank statement, Bank slip, pamoja na ‘Mandate file’

Wamesema nyaraka zingine kama barua kutoka Takukuru m hawana shida nazo lakini wanaiomba busara ya mahakama kuzikataa kwa kuwa zilitolewa zote kwa pamoja na nyaraka ambazo wameziwekea pingamizi.

Hata hivyo pingamizi hilo limepingwa vikali na Upande wa Jamhuri, kupitia Wakili Tarsila Gervas, amesema ushahidi wote ulielezwa na shahidi akiwa chini ya kiapo ulielezea namna mfumo aliofanyia kazi ulivyokuwa imara kwani alijiridhisha kwa huhakikisha kilichopo kwenye mfumo na kile alichoshikilia mkononi.

Hata hivyo baada ya mabishano makali ya kisheria yaliyochukua muda mrefu mahakama inatarajia kutoa maamuzi madogo ya kisheria siku ya leo Novemba 17 kuhusu pingamizi hilo juu ya kupokea ama kutopokea nyaraka hizo kama sehemu ya ushahidi.

BY: Fatuma  Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents