Burudani

Megan Thee Stallion kuipeleka lebo yake mahakamani kisa kutoruhusiwa kutoa nyimbo

Megan Thee Stallion na rekodi Label yake ya 1501 Certified Entertainment hali inazidi kuwa mbaya na sasa Megan ameripotiwa kuwa amewasilisha malalamiko Mahakamani kwa msaada zaidi.


Kulingana na nyaraka za hivi karibuni zilizofikishwa Mahakamani zinadai kuwa Megan Thee Stallion analalamika kuwa Lebo yake inamzuia kutoa nyimbo yeke mpya na kundi maarufu la muziki wa Pop Duniani kutokea Korea la BTS na ameomba jaji aingilie kati ili kufanya mambo yawe sawa.

Megan Thee Stallion ameripotiwa kuchukua hatua za kisheria ili apewe idhini na Lebo yake ya 1501 Certified Entertainment kutoa wimbo wake huo mpya, lakini kulingana na nyaraka za Mahakamani alizowasilisha Megan hivi karibuni ni kwamba lebo yake inadaiwa kuwa inafanya kila liwezekanalo kumzuia Megan asiachie wimbo huo aliopanga kuachia Ijumaa hii, Agosti 27,

Watu wa karibu na Megan wanasema kwamba mmiliki wa 1501 Certified Entertainment Carl Crawford hawatamruhusu atoe wimbo huo sababu wanaamini hautakuwa na faida kwake wakati Megan anamini kuwa ataongeza Kwa asilimia kubwa mashabiki Duniani ukizangatia kundi la BTS linaidadi kubwa ya mashabiki Duniani kote Kwa sasa kwenye muziki wa Pop.

Written by @public_figure_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents