Habari

Njaa Madagascar, chakula hamna watu wanakula wadudu

Madagascar iko katika ukingo wa kukumbwa na ”njaa inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa”, kulingana na Umoja wa Mataifa ambayo inasema maelfu ya watu tayari wanakabiliwa na viwango vya juu vya njaa na uhaba wa chakula baada ya kukosa mvua kwa miaka minne.

Ukame huo – mbaya zadi kuwahi kushuhudiwa ndani ya miongo minne – umeathiri zaidi jamii ya wakulima kusini mwa nchi, na kuwa fanya wageukie kula wadudu ili kuishi.

Watoto

“Hii ni hali ya njaa inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa sio mizozo,” alisema afisa wa Shirikala Chakula la Umoja wa Mataifa, Shelley Thakral.

UN inakadiria kuwa watu 30,000 kwa sasa wanabiliwa viwango vya juu vya uhaba wa chakula uliotambuliwa kimataifa – na kuna wasi wasi kwamba idadi ya walioathirika ikaongezeka pakubwa wakati Madagascar inaingia ”msimu mwembamba” kabla ya mavuno.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents