BurudaniUncategorized

Mfahamu mpenzi mpya wa Wema Sepetu na walivyokula bata nchini Burundi (Picha)

Stori kubwa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu Wema Sepetu na mpenzi wake mpya aitwaye Partick. Mrembo huyo aliacha tabia ya kupost picha za wapenzi wake toka alivyoachana na mchekeshaji Idris Sultan.

Wiki hii amemtambulisha mpenzi wake huyo kupitia Instagram na kuandika ‘my future husband’ kauli ambayo iliwafanya wadau mbalimbali kutaka kumjua mwanaume huyo kiundani zaidi ndipo mtandao wa Bongo5 tulivyoamua kulifungia kazi suala hilo.

Mtandao huu ulita picha ambazo zinathibitisha kwamba Wema Sepetu alikuwa nchini Burundi siku chache zilizopita pamoja na mpenzi wake huyo ambaye pia anatajwa kuwa ana asili ya Burundi.

https://www.instagram.com/p/BpEIBd_nCK_/?taken-by=wemasepetu

Video ambayo amepost Wema Sepetu alionekana kula denda na mpenzi wake huyo imeonekana imerekodiwa nchini humo kwa kuwa nguo ambayo alivaa alipaganayo picha na mastaa mbalimbali wa Burundi.

Hata sauti ambayo zinasikika wakati wanarekodi video hiyo, wanasikika watu wakiongea lugha ya Kirundi.

Akiongea na Bongo5 mtangazaji wa kituo kimoja cha redio cha nchini humo aitwaye, Avec IsmailNiyonkuru alisema wanamfahamu mpenzi huyo mpya wa Wema Sepetu.

“Huyu jamaa tunamfahamu sana kwa jina la Partick na hivi karibuni alikuwa na Wema Burundi, huku ana ndugu zake kwa hiyo huwa anakuja mara kwa mara,” alisema mtangazaji huyo.

Pia mtangazaji huyo alidai mwanamke anayesambaa mtandaoni kwenye akiwa na mpenzi huyo mpya Wema Sepetu ni raia wa Burundi.

Kwa upande wa Wema mapema Alhamisi hii alisema anampenda sana mpenzi wake huyo na hawezi kusikiliza kauli ya mtu yeyote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents