Habari

Mfahamu msichana, Harnam Kore anayehamasisha watu kujiamini na kujikubali kutokana na vile walivyo

Harnam Kore ni mwanaharakati na mzungumzaji katika kampeni kadhaa zinazolenga kuwasaidia watu kukubali maumbile yao, kujiamini na kupona uonevu na unyanyasaji.

Harnam Kore

Harnam anajivunia uso wake uliojaa ndevu, akijifunza kujivunia tofauti yake kwa njia inayopendeza. Anaangazia uzoefu wake, mafanikio yake na kwa nini anastahili matokeo aliyopata.

Mimi ni nani?

”Nimeishi maisha yangu yote kama msichana mwenye ndevu tangu nilipokuwa na miaka 16. Nikiwa na umri wa miaka 12 , nilipatikana na hali inayojulikana kama Polycystic Overy Syndrome, ambayo husababishwa na ukosefu wa usawa wa homoni mwilini hatua ilionifanya kumea ndevu.” amesema Kore

Harnam Kore ameongeza ”Hata hivyo sikuruhusu ndevu zangu kumea hadi miaka kadhaa baada ya kunyanyaswa na wanafunzi wenzangu na watu nisiowajua barabarani. Nilikabiliwa na changamoto wakati nilipokuwa kijana kuhusu kujiamini kwangu na mwili wangu kutokana na umbo langu lisilo la kawaida.”Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu

”Sijawahi kuona mtu anayefanana nami katika runinga. Niliona kwamba kulikuwa na makosa katika mwili wangu, Nilikuwa msichana mdogo niliyekuwa na ndevu na kile nilichotaka kufanya ilikuwa kuonekana mtu wa kawaida.”

”Nilianguka mara tisa, mara ya 10 nikajikukuta na kuvuta pumzi na kugundua kwamba jamii inahitaji kubadili tabia kuhusu maana ya urembo , maana ya kuwa mwanamume, mwanamke ama mtu.”

”Niligundua kwa haraka kwamba nguvu zangu zinatokana na kujiamini. Jamii hii inahitaji mtu mwaminifu aliye mkweli ili kuendelea. Hivyobasi niliamua kuwachilia ndevu zangu na kupambana na ulimwengu jinsi ulivyo.”

”Hicho ndicho kilichokuwa kitu kigumu zaidi kwa mimi kuwahi kufanya. Kila siku, nilijiambia Enua kichwa chako , tabasamu na uwe mtu mzuri. Mwili wangu unanisaidia kuishi na kuwasaidia wengine. Sina nguvu ya kubeba mwili wangu na vile nilivyo.”Kor anapenda alivyo na anasema hajawahi kuona mtu anayefanana naye

Siri ya kujipenda mwenyewe

”Kwa kawaida sisi wenyewe hujipatia shinikizo kali ya kuafikia kiwango ambacho tunajipenda , ijapokuwa kile tunachohitaji kufanya ni kuwa wakarimu kwetu na kwa wengine.”

Mwili wako ni wako wa kuupenda na kuusherehekea .

Waondoe wale waliopo katika orodha yako ya marafiki katika mitandao ya kijamii wanaodhani kwamba haufai kuishi maisha unayoishi na wale katika maisha ya kawaida ambao wanahisi unahitaji kubadilika na sio kuwa ulivyo.

Una maisha yanayoisha hivyobasi unahitaji furaha yote. Watu watakupenda punde wanapokukubali jinsi ulivyo. Wacha nikuwache na wazo hili la mwisho: Iwapo maneno unayojiambia yanaonekana katika ngozi yako baada ya kuyafikiria ama kuyatamka je ni maneno gani utakayotumia kujielezea wewe mwenyewe?

Je utapata wapi usaidizi

Iwapo umepata uzoefu kutoka katika kile unachosoma, ni vyema kuzungumza na mtu unayemuamini kuhusu matatizo utakayokabiliana nayo yawe makubwa ama madogo.

Hatahivyo inaweza kuwa vigumu kuzungumzia kuhusu maumbile ama maswala ya afya ya kiakili.

Lakini kuna mambo ambayo yanatuathiri sote. Iwapo unakabiliwa na ugumu wowote usione aibu ama kuhisi kwamba unahitaji kujificha.

Kuzungumza na daktari ama maatalam wako wa kiafya kunaweza kukuunganisha na watu unaowahitaji kukusaidia na kutoa usaidizi ambao unaweza kubadili maisha yako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents