Michezo

Mfahamu Mtanzania anayekipiga timu ya taifa Uingereza; ”Nafahamu Simba SC ndiyo bingwa wa ligi Tanzania” (+Video) 

Haji Suleiman Mnoga ni kinda wa Kitanzania mwenye uraia wa Uingereza anayekipiga kwenye klabu ya Portsmouth.

Alivyozungumza na ZSports Tv kutoka visiwani Zanzibar, mchezaji huyo amezungumzia juu ya namna anavyoifahamu miamba ya soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC ”Nafahamu Simba SC ndiyo bingwa wa ligi kuu Tanzania.”

Mnonga mweye umri wa miaka 17, anayecheza nafasi ya beki wa kati na kulia ni mzaliwa wa Portsmouth wakati baba yake mzazi akiwa Mtanzania kutoka visiwani Zanzibar huku mama yake akiwa ni Muingereza.

Februari 10 mwaka 2019 kinda huyo alipata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Uingereza ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ikiwa ni kwa mara yake ya kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents