Habari

Mfahamu zaidi Jackie Cliff kwa video hii aliyokuwa akimzungumzia marehemu Ngwair

Jacqueline Clifford Fitzpatrick ni mrembo na video vixen maarufu sana nchini. Umaarufu wake umeongezeka zaidi siku za hivi karibuni baada ya kuenea kwa taarifa za kukamatwa kwake huko Macau, China na madawa ya kulevya aina ya heroin. Alianza kutambulika kwenye video ya wimbo wa marehemu Albert Mangwair, She Got A Gwan. Pia ameonekana kwenye video ya Diamond, Nataka Kulewa na Kimugina ya Linex.

Tulikutana naye kwenye fashion show ya Ally Rehmtullah, Fashion Avenue iliyofanyika Jumamosi, August 31, Serena Hotel jijini Dar es Salaam na kupiga naye story kuhusiana na masuala kibao ambayo ni pamoja na namna alivyokipokea kifo cha Ngwair, kiasi anachochaji kuonekana kwenye video, uhusiano na jinsi watu wanavyomchukulia tofauti.

“I felt so very bad because sikupata kuhudhuria mazishi yake wala msiba wake,” alisema kumuongelea Ngwair.

“Wakati all that happened mimi nilikuwa nje ya nchi. Nilisijikia vibaya kwasababu at first ni mtu ambaye nilifanya naye kazi. Nilishafanya na watu wengine lakini yeye pia aliniintroduce zaidi kupitia kazi zake. Nilijisikia vibaya kwasababu he was like a brother to me. I wish ningepata chance ya kumuona last time, labda kuna vitu ambavyo ningeweza kuongea naye au kumshauri so that he would have changed na asingepata labda na umauti.”

Kuhusu gharama anazochaji ili kuonekana kwenye video za muziki, Jacky amesema kwakuwa Bongo Flava inafanya vizuri, huchaji gharama kubwa.

“Kama mtu yeyote anataka kufanya video na mimi it’s like from two million,” alisema mrembo huyo ambaye baba yake ni raia wa Uingereza.

Kuhusu jinsi watu wanavyomchukulia tofauti kwa muona anapenda kuuza sura Instagram ili kupata wanaume, Jacky alisema hana mpango huo kwakuwa anaye mpenzi wake anayempenda kwa dhati.

“Mambo mengine, shit happens, I am human being. I have been there, I did it, I did some mistakes lakini right now my life is just in a straight way na sijutii chochote kinachotokea maisha mwangu kwasababu it has to be that way.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents