Habari

Mgonjwa auawa ndani ya Ambulensi na kundi la watu Afrika Kusini

Kundi la watu wa Afrika Kusini lilimvamia na kumuua mgonjwa kwenye gari la wagonjwa kwa tuhuma za kufanya uhalifu, kulingana na idara ya afya ya mkoa wa Gauteng.

Umati huo pia waliwashambulia wahudumu wa afya waliokuwa wakimhudumia mgonjwa katika eneo la Atteridgeville na kuharibu gari la wagonjwa.

Wahudumu wa afya waliitikia wito wa usaidizi wa kimatibabu baada ya mtu huyo kujeruhiwa katika shambulio la umati.

Wakiwa eneo la tukio, walianza matibabu na kujiandaa kumsafirisha mgonjwa hadi hospitali ya karibu.

“Ambulensi ilipokuwa ikijiandaa kuondoka eneo la tukio, watu hao walianza kurusha mawe na kuziba barabara kuzuia gari la wagonjwa kuondoka… walidai haki papo hapo,” ilisema taarifa ya idara ya afya.

Iliongeza: “Kwa bahati mbaya mgonjwa alishambuliwa zaidi akiwa kwenye machela ya gari la wagonjwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents