Habari

Mh. Lissu aweka wazi sababu ya kushambuliwa kwa risasi

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa katika historia nzima ya Tanzania tangu uhuru na kabla ya uhuru haijawahi kutokea tukio la kushambuliwa kwa risasi kama alivyoshambuliwa Septemba 7 mwaka jana eneo la area D mjini Dodoma.

Akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya Nairobi ambapo alikuwa anapatiwa matibabu, amesema, Watu hao walinifuata na bunduki za vita kipindi hadi nyumbani kwake.

“Katika historia nzima ya Tanzania tangu uhuru na kabla ya uhuru kwasababu hatukuwa na Bunge kabla ya uhuru baada ya uhuru haijawahi kutokea watu au kikundi cha watu kuchukua silaha au bunduki kwa nia ya kwenda kuuwa kiongozi wa Kisiasa kwasababu tu ya msimamo wake wa kisiasa, hii ni mara ya kwanza katika historia, mtu au kikundi kupanga njama ya kwenda kuuwa kiongozi wa kisiasa eti ni kwasababu mambo anayoyazungumza ndani na nje ya Bunge watu hawayapendi tukio lililonileta Nairobi hoapitali ni tukio la kwanza ,” Tundu Lissu

“Watu hao walinifuata na bunduki za vita kipindi hicho kilikuwa bungeni, nilipotoka bungeni wakanifuata bungeni mchana kutoka bungeni mpaka nyumbani kwangu saa 7 mchana kwa lengo la kuniua. Kwa mara ya kwanza hiyo imetokea na walipokuwa wakiwa na gari wakachukua silaha zao na kwa dakika chache nilimiminiwa risasi nyingi na walioona gari langu wanasema ina matundu 38 ya risasi zilizoingia katika sehemu mbalimbali za mwili wangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents