Habari
Miaka 60 ya Uhuru Wizara ya Maliasili na Utalii kukutana kileleni
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro, amewataka watanzania kujitokeza kupanda mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.
Hata hivyo Waziri Ndumbaro ameongeza kuwa wizara hiyo imeazimia kupanda kilele cha Mlima Kilimanjaro na watanzania 300 na mpaka sasa waliojisajili ni zaidi ya 120 .
Aidha Waziri huyo mwenye dhamana ameongeza kuwa gharama za upandaji Mlima zimepunguzwa hivyo mtanzania mmoja atalipia shiling laji 8 ambazo zitakidhi huduma zote muhimu kwa siku sita.
Mbali na hayo Waziri Ndumbaro amewaomba watanzania kuwa mabalozi wa mlima Kilimanjaro huku akisisitiza kuwa mlima huo mrefu haupo Afrika bali ni barani Afrika nchini Tanzania
BY: Fatuma Muna