Burudani

Mike Tee ndiye aliyeandika script ya video ya ‘Kiboko Yangu’ ya Mwana FA

Bila shaka unaikumbua video ya ‘Kiboko Yangu’ ya Mwana FA na Alikiba iliyofanyika nchini Kenya na kuongozwa na Kevin Bosco Jr na kutoka January 2015. Script ya video hiyo iliandikwa na rapper Mike Tee ambaye pia ana vipaji vingine vya kutengeneza muziki pamoja na kuongoza video za muziki.

Mike Tee a.k.a Mnyalu ameelezea jinsi ilivyokuwa hadi kumuandikia Binamu script ya video hiyo.

“Ile ngoma nilivyoisikiliza siku hiyo kaja kunisikilizisha, nikamwambia mimi nina prefer nisishoot lakini nataka niiandikie script halafu ashoot mtu mwingine, lakini mimi nitakuwa najicho langu nataka kuona nini ambacho kitashootiwa.” Aliiambia 255 ya Clouds Fm. “Nikamwandikia script pale pale akaniambia yaani script niliyokuwa nafikiria mimi yaani ni tofauti kabisa na kile ulichokifanya, kwahiyo alikubali sana script niliyomuandikia.”

Video ya ‘Kiboko Yangu’ licha ya kuwa kali lakini haijabahatika kuoneshwa na vituo vya kimataifa kama MTV Base na Trace, na tulipomuuliza FA kuhusu hilo alidai kuwa alijaribu kutuma kwenye vituo hivyo lakini hakupata majibu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents