HabariMichezo

Mkanda wa kocha wa Simba Robertinho (+Audio)

Mikanda imekuwa sehemu muhimu ya maisha yetu, historia inaonyesha vazi hili lilianza kuvaliwa kati ya 3300 na 1200 BCE.

Kipindi hiki kilikuwa na maendeleo makubwa ya kiteknolojia, kwani tulianza kutumia zana za ufundi za shaba badala ya mawe.

Shaba ilifungua njia kwa zana na silaha za hali ya juu muhimu kwa uwindaji na aina nyinginezo za shukhuli.

Wakati huu mikanda ikawa muhimu na ilitumika sana kubeba vitu haswa silaha.

‘Double D-Ring’ ni miongoni mwa mikanda ya muda mrefu sana, licha ya kuibuka kwa mitindo mingi lakini thamani yake bado haijashuka sokoni kama ilivyo mingine ambayo huibuka na kupotea.

Mkanda huu ambao umekuwa ukizungumzwa sana katika mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni hapa nchini Tanzania baada ya kuonekana kuwa ukipendwa kuvaliwa na Kocha mpya wa @simbasctanzania Roberto Oliveira ‘Robertinho’ thamani yake ni Shilingi 109,908.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents