Habari

Mke aliyetelekezwa na Rais tajiri wa Gabon Ali Bongo aomba talaka, ni mmarekani anayeishi LA!

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rais wa Gabon anayetambulika kwa wengi kuwa ana mke mmoja anayeishi naye kwenye ikulu ya nchini mwake, ana mke wa pili anayeishi maisha ya tabu nchini Marekani.

0929-gabon-inge-4

Rais Ali Bongo Ondimba aliwahi kuishi jijini L.A. kipindi ambacho baba yake alikuwa rais wa nchini hiyo. Alikutana na mwanamke aitwaye Inge mwaka 1991 na kumuoa miaka mitatu baadaye.

Walipata watoto watatu na waliishi maisha ya kifahari kama kumiliki private jets na majumba ya kifahari. Isitoshe mwaka 2006, Inge aliwahi kuonekana kwenye kipindi cha VH1, ‘Really Rich Real Estate’ – ambako alitaka kununua nyumba yenye thamani ya dola milioni 25 huko Malibu.

https://www.youtube.com/watch?t=161&v=Hst7qHI3ou4

Lakini baadaye baba yake Ali alifariki na yeye akawa rais wa Gabon, na kutakiwa kurejea kwao. Inge alimfuata lakini anadai maisha yake kule yalikuwa magumu. Anasema waganga wa kienyeji walimshawishi mume wake kuwa [Ingie] kachanganyikiwa na matokeo yake alipigwa na kutekwa.

Inge alitoroka na kurejea L.A. Ali aliamua kuoa mwanamke mwingine na kukatisha mawasiliano na Ingie pamoja na kuacha kumsaidia kiuchumi.

Inge anasema hajawahi kupokea hata senti kutoka kwa mumewe tangu mwaka 2008.

Na sasa September 2015 … Inge, anayesema anaishi kwenye mazingira magumu anataka apewe talaka. Kwenye nyaraka za mahakamani ambazo mtandao wa TMZ umedia kuzipata, Inge anasema yeye na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 16 wanaishi kwenye nyumba ya kupanga wanayolipia $524 kwa mwezi.

Anataka kupewa fedha za kujikimu na kumlea mwanae.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents