Habari

Mkuu wa majeshi afukuzwa kazi Sudan Kusini

Rais Salva Kiir wa Sudan kusini amemfukuza kazi mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Paul Malong.


Rais wa Salva Kiir wa Sudan Kusini

Jenerali Malong anaonekana na raia wa Sudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo. Hata hivyo mpaka sasa hakuna chombo chochote cha serikalini nchini Sudan Kusini kilichotoa sababu ya kufukuzwa kiongozi huyo.


Jeneral Paul Malong

Katika siku za hivi karibuni maafisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu na pia wengine kutoka serikali ya Sudan Kusini.

Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameiingiza Sudan kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents